Description
Niliwasikia wakizungumza bila kujua ninawasikia. Moyo wangu,mdogo ulivunjika kabisa, kwani siyo tu nilikuwa na ndoto za,kuwa muimbaji, bali pia mimi nilijiona naweza kuimba. Ndugu zangu,wengi wakubwa walikuwa waimbaji, wengine walikua waimbaji wenye,umaarufu kwa miaka hiyo, mfano mzuri ni kaka yangu David Nkone,,na nilijivuna kwamba familia yetu ni ya waimbaji, nikiwemo mimi.,Nilijifunza kupiga vyombo vya muziki mapema, kama ilivyo kwa,watoto wengi wa wachungaji, lakini siku pekee nilizopewa fursa ya,kupiga ni siku ambazo hakukuwa na mpiga mziki kabisa. Kama,ningeanza kupiga ni kwa sababu hakukuwa na mpigaji, au wamechelewa,,halafu baadaye akija kwa kuchelewa, ningeweza hata kutolewa kwenye gitaa katikati ya kipindi cha sifa.
Nilijaribu kupuuza kuhusiana na,upigaji mziki, lakini nilipojiunga kwaya, nilikuwa na matarajio ya,kukubalika zaidi. Kuwasikia viongozi wakisema hivyo, sijui kama,unaweza kuelewa ilinivunja moyo kwa kiasi gani, ila haikunizuia,kuendelea kuimba. Nilikusudia kumtumikia Mungu, nilijua nina wito,ndani yangu, lakini sikujua ni eneo gani haswa. Nilihisi nimeitwa,kuimba hasa kulingana na wenzangu wengi kuwa waimbaji. Kiu ya,kumtumikia Kristo ilinipa maono ya kuwa muimbaji wa kimataifa,,hivyo kujiunga na kwaya ilikuwa ni hatua ya msingi kwa kuanzia.
Reviews
There are no reviews yet.