Showing all 2 results
-
Mara nyingi tulipokuwa kwenye mazoezi ya kwaya, sikuhesabiwa kama,mmoja wa waimbaji. Nakumbuka mara kadhaa wana kwaya,wakihesabiwa, nilirukwa kama mtu asiyekuwepo. Hakukuwa na mtu,wa kuelewa hisia za kuvunjika moyo nilizopata, kwani hata baba yangu,aliyekuwa ndiye Mchungaji, alichukulia ni kitu cha kawaida. Nadhani,kama Mchungaji, hakutaka kuonyesha namna yoyote ya kunikingia,kifua, kwani ingeonekana ni kwa sababu mimi ni mtoto wake.
Akili inanishawishi huenda sina faida katika ufalme wa Mungu, na,labda wenzangu ndio waliobarikiwa na wenye fursa ya kumtumikia,Mungu. Kama mtu angeniambia miaka kadhaa ijayo utakuwa,mchungaji wa kanisa lenye hadhi ya kimataifa, hakuna namna,ningemuelewa.